
Uzinzi na uasherati ni lango la mapepo ndani ya mtu!!
Unapofanya uzinzi au uasherati baada ya kuzaliwa mara ya pili, au unapojihusisha na mahusiano yoyote ya kipepo, hapo tayari unakuwa umejiuza kwa shetani moja kwa moja.. Na hicho ndicho kilichomwangusha pia Samsoni…Biblia inasema katika Mithali 31:3 “Usiwape wanawake nguvu zako;…”. Na inasema pia..
“Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”. 1Wakorintho 6:18 “
Hapo inasema, ikimbieni sio ikemeeni…
Siku hizi ni fashion kila kijana kuwa na girlfriend, na binti kuwa na boyfriend, tena hayo yanafanyika kanisani, na kila mtu anajua..halafu huyo huyo analalamika siku hizi nguvu za kusali zimeisha, anasumbuliwa na mapepo, anaota ndoto mbaya, akisoma neno dakika mbili anasikia usingizi, anashindwa kujizuia kutenda dhambi, mambo yake hayaendi sawa n.k..Sasa hizo nguvu zitatoka wapi wakati tayari umeshampa shetani?…tayari shetani kashakata nywele zako za kiroho, kwa uasherati wako huo, hiyo nguvu ya kuomba utatolea wapi?, hiyo nguvu ya kusoma neno utatolea wapi, hiyo nguvu ya kwenda kuhubiri utatolea wapi, hiyo nguvu ya kufunga utatolea wapi?, utakemea pepo gani litoke?..kwaufupi katika roho, shetani ameshakupofusha macho na anakusagisha ngano katika gereza lake kama alivyomfanya Samsoni. (Waamuzi 16:21).
Na hatima ya wote wanaofanya uasherati au uzinzi kwa siri, ni ziwa la moto.Ikiwa leo unaishi na mwanamume au mwanamke ambaye hamjafunga ndoa! Mwache haraka sana kama unataka kwenda mbinguni, au mwambie mkafunge ndoa …Ikiwa unaishi na mtu unayemwita girlfriend au boyfriend nataka nikuambie mpo chini ya laana, na endapo mkifa ghafla ni moja kwa moja kwenye ziwa la moto, hiyo ni kulingana na maandiko. Kaa mwenyewe mpaka wakati utakapofika wa wewe kuoa au kuolewa, kama uliweza utotoni kwanini usiweze ukubwani!! Epuka injili za shetani zilizozagaa huko zikikuambia ni ngumu kuishi bila hayo mambo, hizo zote zina lengo la kukupeleka kuzimu.
Bwana akubariki sana, kama hujampa Bwana Yesu Maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo kabla siku zako hazijaisha za kuishi hapa ulimwenguni..kabla haijakaribia miaka utakaposema sina furaha katika hiyo (Mhubiri 12).
Maran atha!.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.