Bwana Yesu asifiwe, Karibu katika kujifunza
Vifungu hivi vitatusaidia kujua jibu kulingana na swali hapo juu
Kutoka 14:28
[28]Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
Tusome tena
Kutoka 15:19
[19]Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Vifungu hivi vinatusithibishia, au vinatuweka wazi kabisa kuwa farao naye alikufa katika yale maji, japo katika habari ya farao haijaweka wazi kama farao alikufa naye katika bahari lakini kwa vifungu hivi tu vinatuthibitishia kuwa naye alikufa katika bahari ya shamu
Mfano ukisoma hapo, kutoka 15:19 mwanzoni hapo anasema'”
Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari” ikituonyesha kuwa farao naye alikuwepo katika msafara huo.
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.