SAUTI YA SHUKRANI NI SADAKA MBELE ZA MUNGU. 

Biblia kwa kina No Comments

SAUTI YA SHUKRANI NI SADAKA MBELE ZA MUNGU. 

  1. Yona 2:9 “Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA”.

Shalom, mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, Taa iongozayo miguu yetu..na mwangaza wa njia zetu…Leo tutajifunza juu ya Kumshukuru Mungu kwa sauti tu.

Unaweza usiwe na kitu cha kushika ili umshukuru Mungu… lakini leo fahamu kuwa, sauti yako tu ni sadaka tosha ukitumia kumshukuru Mungu kwa kila jambo analokutendea, liwe baya au jema kwasababu tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.

1Wathesalonike 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Tutumie vinywa vyetu kushukuru sana zaidi ya kunun’gunika. Usisubiri upate kitu fulani ndio ukamshukuru Mungu…kila siku yatupasa kutoa sauti zetu kushukuru Mungu hata kwa kutuumba. Hebu fikiria ungeumbwa mjusi, au kiumbe kingine!. Kwasababu hiyo basi mshukuru Mungu.

Na kama umepata neema ya wokovu ndio kabisa unapaswa kushukuru kila mara. Maombi yetu mengi yawe ni ya shukrani tu.

Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *