JIHADHARI NA MBWA!!

Biblia kwa kina No Comments

JIHADHARI NA MBWA!!

Wafilipi 3:2 “Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao”.

Mbwa wanaozungumziwa hapo sio wanyama, ni aina ya watu wenye tabia kama ya mbwa.

Tabia mojawapo chafu waliyonayo mbwa ni umalaya, utaona mbwa mmoja anakatiza njiani anatembea na mbwa kumi wakifanya kile kitendo hadharani kabisa wala hawana cha kuogopa. Hiyo ni sifa ya umalaya na hivyo watoto wa Mungu jambo hilo halipaswi kabisa kutajwa kati yetu au kushikamana na watu wa namna hiyo kwa jinsi isivyosawa.

Kumbukumbu la Torati 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili”.

Lakini mbwa wengine tunapaswa kujihadhari nao na kuwa makini nao ni MANABII WA UONGO, Bwana Yesu alisema..

Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni MBWA-MWITU WAKALI”.

Hawa sio mbwa tu bali ni mbwa-mwitu tena wakali. Hawa tunapaswa kujihadhari nao sana.

Manabii wa uongo ni wachawi wanaologa roho za watu, kutumia maandiko na miujiza ya kishetani, kama ulikuwa unaogopa wale wachawi wanaowanga usiku, basi unapaswa kuwaogopa hawa zaidi ya hao. Wachawi wa kawaida wanaologa kwa kutumia vitunguli na mapepo ya utambuzi hatujaambiwa tujihadhari nao kwasababu katika ulimwengu wa ukristo hao hawana nguvu yoyote. Ukimuona mtu anasema ni mkristo lakini anaogopa hao wachawi basi huwenda bado hajasimama imara katika imani au labda bado ni mchanga..hajajua mamlaka ya Bwana Yesu, siku akijua hataogopa mchawi yeyote hata awe ni mkubwa kiasi gani.

Lakini wachawi wa kuogopwa na kuwanao makini ni manabii wa uongo. Na huwezi kuwatambua kama huna uhusiano mzuri na Yesu Kristo.

Kumbuka manabii wa uongo sio wale tu wanaojihita manabii, lakini hata Wachungaji wa uongo, walimu wa uongo, wanjilisti wa uongo, wanakwaya wa uongo, mitume wa uongo, wakristo wa uongo hawa wote kwa pamoja wanajina hilo hilo la manabii wa uongo. Kwasababu wanadanganya watu kwa nje hali ndani yao ni mbwa-mwitu wakali, wanawadanganya watu kwa nyimbo zao, miujiza yao, mafundisho yao n.k

Tujihadhari na mbwa”

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *