NAO WAKAO KATIKA NCHI WAMELEVYWA KWA MVINYO YA UASHERATI WAKE.

Biblia kwa kina No Comments

NAO WAKAO KATIKA NCHI WAMELEVYWA KWA MVINYO YA UASHERATI WAKE.

Jina la Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia kitabu cha uzima.

Ufunuo wa Yohana 17:1-6 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;

[2]ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

[3]Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

[4]Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

[5]Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

[6]Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

Bila shaka huyu kahaba aliyelevywa dunia kwa MVINYO ya uasherati wake tunajua ni kanisa katoliki… kama hujui nitumie ujumbe inbox nikufafanulie vizuri kuhusu kanisa katoliki. Na awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa hatupo hapa kwa ajili ya kubeza kanisa fulani au kushindana kwa habari ya makanisa kwamba lipi nzuri na baya, lengo la haya mafundisho ni kufunua ukweli watu wa Mungu wajue njia ya uzima na njia ya mauti ni ipi.

Hivyo kama wewe ni mkatoliki au mshirika wa kanisa hili, usijifungie mlango wa maarifa kwa kusema tunachuki na kanisa lako, fuatilia mambo ili uwe huru na Bwana atakusaidia.

Sasa kwa leo hatutaingia sana ndani kumuelezea huyu kahaba mkuu, lakini tutaangalia huu MVINYO YA UASHERATI WAKE anaoelewesha watu wote wakao juu ya nchi ni nini?

Mvinyo hapa inayozungumziwa siyo divai au pombe bali yale mafundisho na sera zake zote, si ajabu Kanisa hili lina nguvu nyingi katika mataifa mengi kwa utajiri wake kwa jinsi linavyotoa misaada na miradi mingi ya kimaendeleo na ya kijamii, linajenga mashule na mahospitali linatoa misaada ya majanga na kusapoti siasa za nchi, linafanya hivi kwa lengo moja tu! kupumbaza mataifa na wafalme wa nchi ili kuwalewesha kwa kupenyeza mafundisho na itikadi zake za uongo kwa watu ambazo zipo nje ya MANENO MATAKATIFU YA MUNGU.

Na ndio maana tunaona mwanamke huyu ana jina limeandikwa kwa SIRI katika kipaji cha uso wake “BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI”..Umeona hapo, jina lake lipo katika SIRI, hivyo inahitaji HEKIMA kumtambua, kwasababu shetani huwa hafanyi vitu vyake kwa wazi wazi, anatumia kivuli cha “orijino” ili kuwadanganya watu.

Hivyo ndugu, ni vizuri kufahamu haya ili ufanye uamuzi sahihi wa kutoka katika mafundisho haya (mvinyo) yanayokufanya upoteze fahamu kwani biblia inasema “Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.” (Hosea 4:11).

Mafundisho yote yasiyomfanya mtu kuwa mtakatifu bali inamfanya mtu kuwa vuguvugu na kuupenda ulimwengu hiyo ni mvinyo kutoka kwa yule kahaba…na mwisho wa kunywa hiyo mvinyo ni kupoteza ufahamu na kushindwa kujitambua kabisa..na hiyo ndio ajenda ya ibilisi katika nyakati hizi za mwisho.

Biblia inasema kanisa la Laudikia ambalo ndilo kanisa la mwisho ni kanisa lililo vuguvugu na ambalo linajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini, ni kipofu na UCHI. (Ufunuo3:15-18)

Ni kwasababu gani halijioni kuwa ni maskini, na kipofu na uchi? ni kwasababu limepoteza fahamu baada ya kulevywa na ule mvinyo wa yule kahaba.

Ikiwa leo unatembea uchi barabarani, unavaa vimini, suruali, nguo za kubana na kuchora mwili wako, na huku huoni upo uchi, basi tambua kuwa ufahamu wako umeondolewa na hayo mafundisho kutoka kwa yule kahaba mkuu.

Sio ajabu leo hii watu hawatambui majira na nyakati hizi kuwa ni za hatari sana.. ni kwasababu wameleweshwa na mvinyo hawajitambui tena!

Hivyo ndugu: Angalia aina ya mafundisho unayofundishwa mahali ulipo; je! yanakufanya kuwa mtakatifu au yanakupeleka kuupenda huu ulimwengu ambao unaenda kufika mwisho karibuni.

Jihadhari na mafundisho ya uongo! na yale yanayokufanya tu uone vitu vya kidunia na vile vinavyokuja huoni, maana yatakuondolea ufahamu na mwisho utajikuta upo uchi pasipo kutambua kuwa uko hivyo. (Hizi ni siku za mwisho unyakuo wa kanisa upo karibu)

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *