
UNAONA FAHARI JUU YA NINI??
Wagalatia 6:14 “Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ILA MSALABA WA BWANA WETU YESU KRISTO, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu”.
Wapo watu wanaona fahari juu ya elimu zao, nyumba zao nzuri, magari yao ya kifahari, waume zao, wake zao wazuri, watoto wao warembo, wengine ni uzuri wa miili yao wanaona fahari, wengine ni simu zao nzuri, nguo zao za kifahari, n.k lakini sisi watakatifu wa Bwana tunaona fahari juu ya msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kupitia huo tumepata ukombozi wa roho zetu..
Hata kama tutakuwa na mambo hayo yote ya kidunia…bado fahari yetu ni YESU KRISTO, tunajisifu kwasababu ya yeye tu basi, tunaona fahari kwasababu yake peke yake, tunatembea kwa ujasiri si kwasababu ya mali au mtu fulani, bali ni kwasababu ya huyu mkuu wa Uzima Yesu Kristo Bwana wetu, hatutishwi na kitu chochote kwasababu tunaye Mkuu wa Wafalme wa dunia Yesu Kristo, tukipendeza ni kwasababu yake peke yake tu wala si kwa ajili ya mwingine, kila kitu tulivyonavyo iwe ni akili, maarifa, heshima, ndoa, watoto, magari, nyumba, mali n.k ni kwasababu ya yeye tu, hivyo tunamsifu yeye daima, na hata hivi vyote tulivyonavyo vikiondoka bado furaha yetu ipo kwa Yesu Kristo MUNGU WETU MKUU kwasababu havina nafasi ndani ya mioyo yetu.
Halikadhalika tukiitwa washamba na wajinga kwasababu ya kuvaa magauni marefu yasiyobana hatuna shida kwasababu tunafanya hivyo kwasababu ya YESU, kama hatuna akili ni kwasababu yake, tukidharauliwa na walimwengu hatuna shida maadamu tunaye Mwokozi wa ulimwengu YESU KRISTO, ambaye kupitia msalaba wake ulimwengu umesulibiwa kwetu na sisi kwa ulimwengu. Hivyo sisi si wa ulimwengu huu, hatuna urafiki nao..ndio maana hatuvai kama wavaavyo, hatujipambi kama wajipambavyo, hatufurahii vitu vyake kama kushabikia mipira, miziki, mafilamu, vichekesho vyao maana ni uchafu katika ufalme wa Bwana wetu YESU, hivyo sisi na huu ulimwengu ni maadui na mkuu wa ulimwengu huu (shetani) amekwisha kuhukumiwa.
Je wewe ni mwana wa ulimwengu huu au mwana wa Mungu?? Je ulimwengu umesulibiwa kwako? unaona fahari juu ya nini??
Zaburi 20:7-8 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
[8]Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama”.
Bwana Yesu akubariki kwa baraka zote za rohoni na mwilini.
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.