PIGENI MBIO NAMNA HIYO.

Biblia kwa kina No Comments

PIGENI MBIO NAMNA HIYO.

“1Wakorintho 9:23-27 “Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

[24]Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? PIGENI MBIO NAMNA HIYO, ILI MPATE.

[25]Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

[26]Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;

[27]bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.

Safari ya wokovu ni kama mashindano ya riadha!, kila mmoja anapiga mbio kuelekea ukamilifu, na kama tunavyojua wanariadha wanaanza wakiwa wengi lakini mshindi ni mmoja tu, hivyo kila mwanariadha anapambana kweli kweli kuakikisha anakuwa wa kwanza. Na hivyo hivyo katika Imani wakristo ni wengi lakini watakaoshinda ni wachache tu wale waliopiga mbio kweli kweli. Ndio maana ukisoma yale makanisa 7 katika ufunuo 2-3 unaona kila kanisa mwishoni Kristo anamalizia kwa kusema yeye ashindaye atapewa dhawabu fulani, kwa mfano tuangalie kanisa letu la Laodikia,

Ufunuo wa Yohana 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.

Umeona “yeye ashindaye” maana yake ni mashindano, ndio maana Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho aliifananisha safari ya ukristo na wanariadha, akasema tupige mbio kama wao, na ili tuweze kupiga mbio vizuri ni lazima tujizuie na mambo mengi ya kidunia, tujizuie na fashion na mitindo ya kidunia, tujizuie na kampani za watu wenye mizahaa, makundi mabaya, tujizuie na mambo yote ambayo yatatupelekea tushindwe kupiga mbio vizuri katika kuomba, katika kusoma biblia, katika kumtafuta Mungu..ikiwa ni mitandao tujizuie tusitumie muda wetu kukesha huko kufuatilia vitu visivyojenga roho zetu, ni afadhali tutumie huo muda kukesha kusoma biblia, au kuomba.

Pia hatupaswi kusongwa na kulemewa na masumbufu ya maisha tukasahau tupo katika mashindano, mkristo hapaswi kukosa saa moja ya kuomba ndani ya siku kisa kazi imembana ni heri aache hiyo kazi, au akose ibadani kwasababu sisizo na maana… sababu sababu ndio itawafanya wengi washindwe kushinda na kuachwa na Bwana!! Weka kila mzigo kondo unaokuzuia kupiga mbio… unyakuo umekaribia sana!!

Waebrania 12:1-2 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

[2]tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”.

Weka kando mzigo wa umbeya, weka kando mzigo wa uasherati, weka kando mzigo wa ulevi wa mambo ya kidunia.

Bwana Yesu yupo mlangoni kurudi!!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *