UPUMBAVU WA MUNGU UNA HEKIMA ZAIDI YA WANADAMU.

Biblia kwa kina No Comments

 

UPUMBAVU WA MUNGU UNA HEKIMA ZAIDI YA WANADAMU.

1 Wakorintho 1:25 “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

Je! Mungu anao upumbavu? La, hasha, Mungu wetu aliye mkuu sana, yeye ambaye hana mwanzo wala mwisho, ambaye akili zake hazipimiki, na njia zake hazichunguziki hawezi kuwa na upumbavu wala hana udhaifu wowote, lakini kazi zake zimemfanya aonekane kuwa ni mpumbavu kwa wale wanaopotea, wale ambao neno la msalaba kwao ni upuzi.

Ndio maana wasomi wengi, watu wenye hekima ya dunia hii, mambo ya Mungu kwao yanaonekana ni upumbavu, lakini upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wake una nguvu zaidi ya wanadamu. Na yale mambo yaliyoonekana ni ya kipumbavu ndiyo Mungu alivichagu ili kuaibisha wenye hekima ya dunia, wale watu wasio na elimu, wale wasiojulikana, wale waliodharaulika, ndio Mungu anawachagua na kuwatumia ili wale wenye hekima, wenye ujuzi, wenye nguvu wasibwe vinywa.

1Wakorintho 1:26-31 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;

[29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.

[30]Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

[31]kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

Ukweli ni kwamba mtu akiwa nje ya Kristo hana akili, hata kama anao degree zote za elimu, hata kama ni mwanasayansi aliyebobea, kama hana Yesu wa kweli, elimu yake na maarifa aliyonayo ni ubatili. hekima pekee Mungu anayoitambua ni YESU KRISTO ndiyo hekima ya Mungu, hivyo ili mtu aonekane anao akili, anao hekima ni lazima awe na Yesu moyoni mwake na katika maisha yake.

Je! unaye Yesu wa kweli, hekima ya Mungu? Je unaona fahari juu yake? au unaona fahari juu ya elimu yako?

Kama hujampokea YESU kwa kumaanisha kabisa kutubu dhambi na kuziacha, basi wakati wa wewe kufanya maamuzi ni sasa kabla mlango wa neema haujafungwa, muda uliobakia ni mfupi sana.

Maran atha (Bwana anarudi)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *