Fahamu jambo moja ambalo Bwana anataka tu kwako?
Ikiwa unafikiria kumrudia muumba wako, na unashindwa pa kuanzia.
Yamkini unawaza kwamba umetenda dhambi nyingi sana, kiasi kwamba unahisi tayari umeshamkufuru Mungu, na unaona hata ukimrudia hautasamehewa kwa wingi wa dhambi ulizozifanya. Basi leo Bwana anasema nawe kwa neno hili..
Yeremia 3:13 “Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi,…”
Umeona kitu Bwana anachotaka kwako! Ni wewe kuungama tu dhambi zako zote na ukiri ya kuwa wewe ni mkosaji na hivyo ulistahili adhabu ya milele, na sasa umetambua makosa yako na uko tayari kumrudia Mungu wako. Hicho tu ndicho Bwana anataka kwako leo, (anataka tu usarende)!
Useme kuanzia sasa mimi na dhambi basi, mimi na udunia mwisho.
Ikiwa utakubali kusarenda na kumrudia yeye, anasema sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema.
Hebu soma Isaya 1:18 Bwana anasema..
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Haijalishi umetenda dhambi nyingi kiasi gani, yawezekana ulitoa mimba sisizo na idadi, umebadilisha maumbile yako mpaka rangi ya ngozi yako, haijalishi umemwaga damu nyingi za watu kiasi gani, haijalishi umezini na waume au wanawake wangapi, au umedhulumu watu wengi kwa namna gani n.k. Unachotakiwa kufanya ni KUUNGAMA TU! NA KUACHA maovu yote pasipo kuficha au kuacha hata moja. Kwani biblia inasema…
Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziuangamaye na kuziacha atapata rehema.
Leo kubali kuangama dhambi zako na kumaanisha kuziacha kabisa upate msamaha bure. Na kupewa kufurahia mema ya nchi (baraka za Mungu), na zaidi uzima wa milele.
Lakini kama ukikataa basi, Bwana anakuambia…
Isaya 1:20 bali kama ukikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.
Fahamu kuwa kuna adhabu ya ziwa la moto ambalo wote waliokataa kuungama maovu yao na kumrudia Mungu walipokuwa wakisikia sauti yake ikiwaita watoke kwenye dhambi waje wapokee msamaha wa dhambi bure,…hawatakwepa hiyo hukumu kama wasipokubali kugeuka sasa.
Hivyo ndugu, unayesoma ujumbe huu, yamkini ni wewe ambaye Bwana anakuita leo, uache njia zako mbaya, uache kujiuza, uache kuchafua mwili wako kwa vilevi, uasherati, kujichua, na kuvalia mavazi ya nusu uchi.
Hivyo basi kubali wito huu wa kutubu kabla hii neema haijaondolewa kwako. Wala usihangaike kuhesabu dhambi zako, we kubali tu kutubu na kuachana na ulimwengu.
Bwana atakusamehe kabisa na kukufanya kuwa kiumbe kipya, maana mawazo yake si mawazo yetu.
Isaya 55:6 “Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
Saa ya wokovu ni sasa, usisubirie kesho maana hujui yatakayotokea hiyo kesho. Chukua hatua sasa hivi mgeukie Bwana bila kusita sita.
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.