Unataka Mungu akutumie?
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Ukweli ni kwamba Mungu anatamani sana kufanya kazi na sisi na sisi pia tunatamani sana kufanya kazi na Mungu na ajidhihirishe kwetu ulimwengu umgeukia kama libido cha baba zetu(Mitume) lakini kuna mambo ambayo yanamzuia Mungu kufanya kazi kikamilifu na sisi.
Na Mungu anataka kumtumia kila mtu kwa viwango vya juu zaidi na anataka kutuna mambo anataka kutupa makubwa zaidi lakini anapotuangalia kuna viwango bado hatujavifikia yaani hatujawa qualified.
Na bahati mbaya wengi wetu hatufahamu hili, tunajuhudi ya kufunga,kuomba,nk yote ni mazuri na yanafaa lakini nataka tutafakari mambo kadhaa hapa.
2 Timotheo 21
9 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.
20 Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
21 Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.
Nataka tutafakari kwa kina mistari hii hapa tujifunze jambo.
Anasema “…Msingi wa Mungu ulio imara umesimama,wenye muhuri hii,Bwana awajua walio wake kila alitajaye jina la Bwana na uache uovu.” Maandiko yanasema anawajua walio wake ni wakina na nani? Ni wote waliomwamini Yesu Kristo yaani walio na Roho Mtakatifu hao Bwana anawajua ni wake wala hakatai.
Lakini anataka kila wanaolitaja jina la Mungu na wauache uovu(Mimi na wewe tuliookoka) sasa kwa nini anasema hivi katika mistari inayofata anatoa maelezo.
Anazungumzia juu ya vyombo vipo vya dhahabu, shaba, udogo, miti nk lakini anasema vipo vyenye heshima na vingine havina. Mstari unaofata anasema….
Ikiwa mtu amejitenga(kuna kutengwa-pale unapookolewa umetengwa mbali na dhambi umekua kao la Mungu, lakini kuna kujitenga wewe pia mbali na uovu)
Sasa anasema “…amejitakasa kwa kujitenga..” hasemi …”ametakaswa na kutengwa..” maana yake ni wajibu wako wewe pia kujitenga na mambo mabaya. Si kuendelea kuyafanya.
Anasema “….atakuwa chombo cha kupata Heshima kilichosafishwa kimfaacho Bwana,kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema..” kumbe ili uwe chombo cha Heshima kilichosafishwa na kimfaacho Bwana ni wajibu wako wewe kujitenga pia.
Maandiko yanasema ikiwa Mtu maana yake si mchungaji tu,mtume,nabii,muinjilisti,shemasi,mzee wa kanisa, nk bali ni yeyote yule kama akiwa ni mtu wa kujitenga na uovu basi Bwana ni lazima atamtumia tu kwa kila kazi njema.
Ikiwa unataka uone kweli Mungu akitembea na wewe akutumie basi fanya juu chini kuepukana na uovu, matusi, mizaha,uzinzi,tamaa mbaya,mazungumzo mabaya,uasherati, nk ikiwa unayafanya moja wapo au yote yaepuke.
Wewe ni mtiwa mafuta wa Bwana na Yesu anataka akutumie katika viwango vikubwa ssna imalisha with wako.
Ishi maisha matakatifu utaona faida nyingi sana na sio hasara. Usiishi tu kama Mkristo uliyeokoka lakini upo upo tu kataa hiyo hali Ukristo ni maisha, jinsi unvyokuwa kanisani husemi matusi wala kufanya mambo mabaya ndio uhalisia wako unabidi uwe nao mpaka nje ya kanisa. Usiwe mnafiki kanisani uko hivi nje na kanisa uko hivi.
Nimekuombea kwa jina la Yesu Kristo neema iongezeke kwako uwe chombo kimfaacho Bwana kwa kila kazi njema na chochote kinachokuzuia katika Jina la Yesu kimetoka, Bwana akuimalishe.
Ubarikiwe sana.
Maran atha.
Mawasiliano:0613079530
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.