
KIMBIENI KUTOKA KATI YA BABELI.
Isaya 48:20 “Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
Tukisoma kitabu cha Danieli tunaona kuna habari ya mfalme mmoja aliyeitwa Nebukadreza, huyu alikuwa ni mfalme katika dola ya Babeli ambayo ilikuwa ni dola kubwa sana hapo kale, ndio iliyohusika kuwachukua wana wa Israeli utumwani miaka 70, lakini baadaye ilikuja kuangushwa na dola zingine kama tunavyosoma katika historia.
Sasa huyu mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli akiwa katika utawala wake alitengeneza SANAMU kubwa iliyo na mfano wa mtu na kuiamuru watu wote waiabudu wakiwemo wana wa Israeli. Kumbuka Mungu aliwapa wana wa Israeli sheria na amri kwamba wasiabudu sanamu wala kitu chochote chenye mfano wa umbo lolote.
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”
Hivyo Mfalme aliposikia habari yao alighadhibika na kuwatupa katika tanuru la Moto, lakini tunaona Bwana aliwaokoa na ukali wa moto ule.
Lakini huyu mfalme yeye hakujali hiyo amri ya Mungu, bali aliwalazimisha watu wote waisujudie sanamu yake na kwamba mtu yeyote asiyeisujudu atatupwa katika tanuru la moto.
Danieli 3:1-6″ Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,
5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Lakini pamoja na hayo walionekana watu baadhi waliokaidi amri ya mfalme nao ni Meshaki, Shedraka na Abednego. watu hawa tunasoma walikuwa ni wacha Mungu tangu awali, tunaona walikataa kula vyakula najisi vya mfalme, na hapa pia wanakataa kuabudu sanamu ambayo ni kinyume na sheria ya Mungu aliyowapa, kwa mkono wa Musa kule jangwani.
Kumbuka Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya,(wakolosai 2:17) yaliyotokea katika mwili agano la kale, ndiyo yanayoendea sasa katika roho kwenye agano jipya, na ndio maana tunaona hapa inatajwa BABELI ya NJE, lakini tukisoma katika kitabu cha Ufunuo 17 &18 Tunaona inatajwa BABELI nyingine. Hivyo tabia inayojitokeza kwenye hiyo ya mwilini itafanana na hii ya rohoni.
Na kama Babeli ile ya kwanza ilivyounda sanamu na kulazimisha watu wa dunia nzima waiabudu na yeyote asiyeabudu atatupwa katika tanuru kali la moto, vivyo hivyo na hii ya rohoni inaunda SANAMU yake na mtu yeyote atakayekaidi kuiabudu, adhabu yake itakuwa ni mateso ambayo biblia inasema hayajawahi kuwepo tangu dunia kuumbwa (DHIKI KUU)..Habari hii tunaweza kuisoma katika…
Ufunuo 13:15 Akapewa kutia pumzi katika ile SANAMU YA MNYAMA, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao WOTE WASIOISUJUDIA SANAMU YA MNYAMA WAUAWE.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao:
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Kumbuka Mnyama huyu ni RUMI na dini yake ni KATOLIKI, ndio BABELI ya rohoni iliyopo sasa. Itafika kipindi itapata nguvu kwa kuunganisha DINI zote na Madhehebu yote ulimwenguni ili kuunda DINI moja (ambayo ndio SANAMU YA MNYAMA), ambayo pasipo hiyo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa, na yeyote atakayeonekana hana chapa(utambulisho) wake, adhabu yake itakuwa ni mateso makali na vifo. Kama vile amri ya Mfalme ilivyokuwa kali juu ya akina Shedraka mpaka moto ukachochewa mara saba, ndivyo mateso yao yatakavyokuwa makali kwa wale wote watakaokataa kusujudia ile SANAMU ya Mnyama au kupokea CHAPA YAKE.
Ni mambo ya kutisha yanakuja huko mbele usitamani uwepo, anza kuweka sawa mambo yako yahusuyo wokovu leo kabla wakati haujaisha. Huu ni wakati wa kutoka kwenye kamba za madhehebu na kutafuta wokovu wa kweli, madhehebu yote Mungu ameyahukumu, na ndiyo yaliyoibeba ile chapa ya mnyama ndani yake. Neno la Mungu linasema..
“Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
[45]Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.” (Yeremia 51:44-45).
Yeremia 51:6 Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
Toka Babeli, KIMBIA! KIMBIA!, jiokoe nafsi yako.. “Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni”. (Yeremia 51:9).
“Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake”,
Unapousikia ujumbe huu, ufanye hima utoke, na sio utoke kwa miguu au ubadilishe kanisa, hapana bali utoke kwa kuutafuta ukweli na kuoana na neno la Mungu, ujazwe Roho wa Mungu. na Roho ndiye atakayekuongoza katika kuijua kweli yote, sio dhehebu wala shirika lolote la dini wala kanisa, tafuta uhusiano wako binafsi na Yesu Kristo.
Mungu akubariki!
Ufunuo 18:1-5 “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
[2]Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
[3]kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
[4]Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
[5]Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

Maran atha (Na uje Bwana Yesu)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618