KAA MBALI NA UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO.

Biblia kwa kina No Comments

KAA MBALI NA UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO.

2 Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, NA TUJITAKASE NAFSI ZETU NA UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.

Uchafu wa mwili ni upi? Ni matendo yote machafu yanayofanyika katika mwili mfano uasherati, ulevi, usagaji, ulawiti, ufiraji, upigaji punyeto, kutazama picha za ngono/pornography, uvutaji sigara na madawa yote ya kulevya, lakini pia uchafu wa mwili ni pamoja na uvaaji mbaya wa vimini, visiruali kwa wanawake, nguo za kubana/modol kwa wote, kunyoa denge, kusuka nywele, kuvaa wigi, kuchora mwili, kupamba mwili kwa mapambo ya nje mfano kupaka makeups, hina, kutoboa pua na kuweka vipini, kutoboa masikio na kuweka hereni, kupaka kucha rangi, kutia wacha, kupaka mdomo rangi/lipsticks, hivyo vyote ni uchafu wa mwili, hata kusikiliza miziki ya kidunia, kutazama movies, kushabikia mipira, kubeti, kucheza kamari/magemu aina zote, kuperuzi peruzi mitandaoni bila sababu,kuchati chati kihuni, kuwa na mahusiano ya kimapenzi bila utaratibu wa kibiblia, kutukanana, kusengenyana, kusema uongo ni kuchafua nafsi. Unasema mtumishi mbona sasa kila kitu ni dhambi, ndiyo hayo yote ni dhambi na mambo mengine yanayofanana na hayo ni machukizo kwa Mungu, kwa ufupi kuupenda ulimwengu ni kujichafua nafsi.

Lakini pia kuna uchafu wa roho, haya ni matendo machafu yanayofanyika ndani ya moyo wa mtu hayaonekani kwa nje, mfano mawazo mabaya, kutokusamehe, vinyongo, chuki, hasira, uchungu, ugomvi moyoni, matusi moyoni, kunung’unika nung’unika na kulalamika-lamika hovyo, kuwa na unafiki, kiburi, n.k mambo haya hayapaswi kukaa ndani ya mkristo halisi.

Kumbuka hii sio sheria, hapana, ukiona kuna ugumu wa kushinda hivyo vyote na mengineyo basi unahitaji msaada wa Mungu. Na msaada huo unapatikana bure, ni wewe tu kuamua kumpokea YESU wa kweli ambaye atakujaza Roho Mtakatifu, huyu Roho Mtakatifu akiingia ndani yako atakusaidia kuishi maisha masafi bila hata wewe kutumia nguvu yoyote, ataweka chuki ndani yako ya kuchukia ulimwengu na mambo yake yote, hivyo uchafu wowote wa mwili na roho hauwezi kuwa ndani yako kwasababu tayari wewe mwenyewe hautaki uchafu…na umekwisha fumbuliwa macho na kuonyeshwa mambo yote yanayomchukiza MUNGU, hivyo hauhitaji tena kuhubiriwa sana kwamba hiki ni sawa na hiki si sawa, Roho Mtakatifu aliye ndani yako atakuongoza katika kweli yote na kukusaidia..na hivyo utaishi maisha ya amani na utafurahia wokovu, utampenda sana BWANA YESU.

Je umepokea Roho Mtakatifu? udhibitisho ya kuwa umempokea au la, ni jinsi unavyochukuliana na mambo hayo tuliyoyataja kwamba unashikamanavyo au yamewekwa mbali na wewe. Jitathimini mwenyewe na ufahamu kuwa Bwana Yesu anasema wote wasio na Roho wake hao sio wake (Warumi 8:9), hivyo hawawezi kumuona wala kuurithi ufalme wake kwa kuwa hawajazaliwa mara ya pili.

Bwana akusaidie uone hili, na ufanye maamuzi sahihi iwapo bado hujaokoka.

Bwana Yesu anarudi. Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *