Ni kweli njia ni nyembamba na njia imesonga iendayo uzima?.

Biblia kwa kina No Comments

Ni kweli njia ni nyembamba na njia imesonga iendayo uzima?.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Mathayo 7:14“Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”

Bwana Yesu ambae anataka watu wote waokolewe..

2 Petro 3:9“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.”

Soma pia (1 Timotheo 2:4) je! Anaweza kufanya mlango uwe ni mwembamba na njia ya kumfikia yeye iwe ni ya taabu na mateso mengi? Mwisho wa siku watu washindwe kumwamini wafe katika dhambi na waende mbinguni? Au je anaweza kuruhusu Mlango kuwa ni mwembamba?

Ukweli ni ni kwamba njia ya kumfiki Yesu Kristo ni pana wala haijasonga kabisa..

Sasa ni kwa nini Yesu Kristo alizungumza vile?

Ni kwasababu aliona watu wamesongwa sana na shughuli/Mambo ya ulimwengu huu pamoja na udanganyifu wa mali kiasi kwamba hawamuoni Mungu lakini kitu wanachokiona na wanaamini kinaweza kuwapa furaha na amani ni mambo ya ulimwengu huu kama vile Fedha nk.

Watu wengi wanasikia njili lakini hawajawa tayari kuikubali.. na Wakristo wengi pia wamesongwa na mambo ya ulimwengu hata kufanya kile walichopokea hakizai na wengine wanapatwa na changamoto kidogo tu wanamuacha Yesu Kristo hakuna Saburi..

Sasa udanganyifu huo umefanya wasiione njia ya kumfikia Mungu ambae ni Yesu Kristo.

Katika nyakati za Mwisho hizi mtoto hajengewi tena njia ya kumjua Mungu anajengewa misingi ya mafanikio kupitia elimu(siyo jambo baya ni jema kabisa lakini misingi hiyo haiwezi kumfikisha mbinguni ni ubatili kama asipomjua Mungu).

Sasa njia ya kuelekea uzimani ni wachache wanaoiona si kusudi la Mungu watu waione wachache la! Lakini ni wachache wanaosikia sauti ya Roho Mtakatifu ikiwaita… sio kwamba Roho Mtakatifu anasema na wachache la! Bali wengi ila wanaokubali kutii hao ndio wanaokolewa.

Lakini wengi wanasikia sauti ya Roho Mtakatifu na hawatii.. wanakuwa bize na mambo ya ulimwengu huu.

Hiyo kuonekana njia imesonga na ni nyembamba sana na watu wanapotaka kuiendea wanavutwa na udanganyifu na anasa za ulimwengu huu.

Na watu wenyewe wanapenda giza kuliko nuru.. wanaichukia nuru. Wanataka kuendelea kukaa katika uchafu ilihali wanafahamu kabisa nafsini mwao wanatakiwa kutoka gizani huko na waishi maisha yanayompendeza Mungu.

Dhamiri zao zinawashitaki kila siku Lakini wameweka shingo ngumu hawataki kugeuka kama watu wa Sodoma na Gomora na watu wa kipindi gharika ya maji.

Yohana 3 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

20Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.

21Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Watu wanaiona nuru(Yesu Kristo) lakini hawataki kuifata nuru.

Kwa hiari zao wamekusudia kuwa wa hivyo..

Isaya 5:20 “Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!”

Wale wanaopenda kweli siku zote wanataka kurekebika na kutembea katika mwenendo mzuri.. wanatamani kumtafuta

Zaidi Kristo watembee katika mapenzi yake.

Sasa ili tuweze kuipita vyema hii njia hatuna budi kulazimisha kupitia katika njia hiyo ambayo inaonekana ni ngumu lakini sio ngumu maandiko yanasema nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi.

Siku zote mambo ya ulimwengu huu hayapatani na mambo ya Rohoni ndio maana yanaonekana kuwa kama magumu.

Njia hii inaonekana pia imesonga kwa sababu ukiipita utaonekana kama umerukwa na akili lakini maandiko yanasem..

Isaya 35: 8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO”.

Haleluya hakikisho ni kwamba hutapotea japokuwa ulimwengu utakuona umepotea.

Kuna wakati utaona waovu wanastawi wanafanya lolote watakalo na hakuna kinachowapata utaona kana kwamba wanafaidi lakini maandiko yanasema.

Malaki 3:18“Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.”

Soma pia Zaburi 73:3-5.

Hivyo njia haijasonga ni pana na Yesu anataka watu waokolewe..

Nimekuombea kwa jina la Yesu Kristo hutapotea kamwe ijapokuwa utaonekana machoni pa ulimwengu umepotea lakini uhalisia wewe hujapotea bali ni mwenye hekima.

Na ulimwengu ndio umepotea.

Maranatha.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *