UWEZA WA MUNGU HUTIMILIKA KATIKA UDHAIFU 

Biblia kwa kina No Comments

UWEZA WA MUNGU HUTIMILIKA KATIKA UDHAIFU 

2 Wakorintho 12:9 ”Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Tukitaka kuona uweza wa Mungu, tukubali kuwa dhaifu. Udhaifu ninaouzungumzia sio ule wa kuwa na makosa fulani, hapana, huo unaweza ukawanao lakini sio wa kujisifia nao.

Lakini udhaifu ambao Bwana anataka tuwe nao ili tuone uweza wake..ni pale unapokuwa katika hali fulani ya uhitaji na haouni pakutokea, pale unapokwama kwa jambo fulani, pale unapokuwa katika hali ya kuishiwa nguvu, au unapopitia hali ya ukame kiuchumi, unapopitia changamoto ya kiafya, au janga fulani na mambo mengine yote yaliyo juu ya uwezo wako, huo ndio udhaifu ambao mtu akimtegemea Mungu katika hali hizo ataona uweza wake.

Udhaifu ni pale unapokataa kutegemea akili yako, unapokataa kutafuta njia mbadala kutatua tatizo lako ukamtegemea Mungu.

Kwa mfano upo katika hali ya ukame, umeishiwa kabisa..hujui hata ule nini saa hiyo, kila ukiangalia mashariki magharibi huoni pa kutokea, akili zako hazifanyi tena kazi, au pengine mwenye nyumba kakuambia leo ni lazima umlipe kodi yake na wewe hapo hauna chochote kabisa na wala hujui pakupatia, ukishakuwa kwenye hali kama hiyo, basi tegemea kuona uweza wa Mungu…usianze kukimbia kukimbia huku na kule kutafuta msaada kwa watu, au kupiga piga simu kwa kila mtu, we tulia mwamini Mungu maadamu tu unayafanya mapenzi yake..nakuambia Mungu sio muongo utaona tu uweza wake ukikusaidia hapo ulipokwama, utashangaa tu mlango unakufungukia kwa njia ambayo hata hukutarajia.

Mwingine ni mgonjwa..ukishakuwa katika hali hiyo usipende kutafuta tafuta msaada kwingineko kwasababu hautakaa uone uweza wa Mungu, ni kweli unaweza ukatatua shida yako kwa namna yako wewe, lakini ni lini utamuona Mungu, kwanini usitumie tatizo lako kumuona Mungu ukasema mimi sihangaiki acha Mungu anisaidie mwenyewe, shetani atakuletea mawazo kwamba fanya hivi na hivi, wakati mwingine utaona ni kama akili yako inakushauri uchukue uamuzi fulani ili ujisaidie lakini ni lini utaona uweza wa Mungu…kwanini usikubali kusurrenda kwa Mungu, kwa ufupi tunapaswa kuwa kama vitoto vidogo kwa Mungu visivyoweza kujisaidia kwa lolote hata kama tunao uwezo… tunapaswa tuwe wadhaifu kwa Mungu.

Kumbuka hapa sijazungumzia mtu akalale ndani bila kujishughulisha na kazi yotoye, iwe ni kazi ya Mungu au kazi yake mwenyewe halafu akae asubirie uweza wa Mungu umshukie…hapo utaangamia kwa kukosa maarifa. Lakini kwa ujumla uweza wa Mungu hutimilika katika udhaifu.

2 Wakorintho 12:9-10 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ILI UWEZA WA KRISTO UKAE JUU YANGU.

[10]Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. MAANA NIWAPO DHAIFU NDIPO NILIPO NA NGUVU.”

Neema ya Mungu yatutosha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *