Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi wetu.
“Mungu kukaa kimya haimanishi kwamba hayupo au hayuko na wewe..” kiwango anachotupimanacho Mungu cha uaminifu ni yeye kukaa kimya kwa kipindi fulani.
Katika maisha ya wokovu kuna wakati Mungu anasema na sisi mara nyingi sana katika mambo mbali mbali ikiwemo maonyo ya wazi wazi pale tunapokosea. Anatuonya ili tubaki katika njia ya haki.
Lakini kuna nyakati Mungu hukaa kimya kabisa katika maisha yetu ya wokovu unapofanya kosa huoni akikuonya.. alikuwa anasema na wewe katika mambo mbali mbali hasemi na wewe tena, ulikuwa unahisi uwepo wake kila wakati Lakini inafikia hatua ni kama huoni uwepo wake tena.. unaona kana kwamba hayupo. Amekuacha uko mwenyewe nk.
Ulikuwa unasikia bubujiko ndani yako unapokuwa katika maombi. Unaposoma neno, unapokwenda ibadani Ulikuwa unaona bubujiko la kweli la Mungu ndani yako. Lakini kuna wakati unafika unaona ukame wa hali ya juu unaomba Lakini kana kwamba unaona Mungu hakusikii kabisa na hayupo.
Unaanza kuhisi wakati mwingine kuwa Mungu kakuacha hayuko na wewe tena unaanza kuomba toba na rehema unajitakasa na kuanza kukumbuka makosa ya nyuma unatubu Lakini huoni kitu chochote yaani ni ukame wa hali ya juu.
Sasa katika kipindi kama hiki watu huwa wanapoa na kujikuta wanaanza kurudi nyuma taratibu taratibu tu.. ni kipindi cha kuwa makini sana.
inafikia hatua unafanya makosa Lakini kwa sababu huoni Mungu anakukemea wala huoni maonyo yoyote unajikuta unaanza kuyachukulia kawaida tu(unamuona Munguni kama wewe tu na anachukuliana na uovu wako) unasema “maandiko yenyewe yanasema sisi ni wadhaifu….” ndugu si wadhaifu wa kutenda dhambi Tena huku unaelewa kabisa kuwa ni kosa.” . Unaanza kuona ni mambo ya kawaida lakini sivyo.
Unaanza kuangalia picha za uchi leo(na unasema umeokoka kabisa) Mungu anakaa kimya unachukulia ni kawaida tu na kesho unarudia mwisho inakuwa ni tabia yako.
unazini leo unaona Mungu yupo kimya unarudia tena na tena unajisemea ” ni Hali za mwili tu Mungu anajua aturehemu tu” Mungu ni mwenye rehema kweli lakini si katika upumbavu.
Hivyo tabia chafu zinaendelea kuzalika ndani yako Unadhani Mungu hayupo karibu na wewe au ameshakuacha au unaona Mungu anachukuliana na wewe kuwa ni dhaifu lakini sivyo hivyo kabisa.
Zaburi 50:16 “Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.
20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya”
Unaona hapo kwenye mstari wa 21? Anasema.. “Ndivyo ulivyofanya nami nikanyamaza…” anaendelea kusema “…..ukadhani ya kuwa mimi ni kama wewe…”
Hivyo katika kipindi hiki ni kuwa makini kabisa.. Mungu anapokaa kimya si kwamba haoni ama hajui ama anachukuliana na upumbavu la!
Bali anachotaka ni wewe ujitambue wala hatakaa siku zote anakuonya kuna kipindi kitafika(utu uzima wa rohoni) anatarajia wewe mwenyewe ujitambue na ufahamu kabisa natakiwa kuenenda kama mtu nilie na Mungu ndani yangu wala si kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu.
Usijitumainishe kwa michango unayotoa kanisani.. karama yako nk ndugu hivyo hata manabii wa uongo wanavyo(Hata Shetani alivyoasi wala Mungu hakumnyanganya Nguvu anazo hata sasa lakini hazina mamlaka kwa mtu anaemfata Yesu Kweli kweli) na karama za Mungu hazina majuto akikupa amekupa wala hakunyanganyi lakini sahau kuhusu Mbingu.. utasema Bwana, Bwana lakini siku ile hatakutambua.
Hivyo kipindi Mungu unapoona kuwa yuko mbali na wewe.. huhisi uwepo wake ndugu yangu usipumbazike na kufikiri Mungu hayupo pamoja na wewe Bali jua kabisa ndio kipindi ambacho Mungu yupo karibu sana na wewe kushinda hata nyakati unazohisi..
Ndio wakati ambao yeye anatazamia wewe mwenyewe usimame na kukataa uovu pasi yeye kusikia anakukemea uache.
Tengeneza leo mahali ambapo hapako sawa kisha tembea na Yesu Kristo hata kama unaona uwepo wake haupo( siku zote Bwana Yuko pamoja na sisi ila fikra zako ndio zinazo kwambia Mungu yuko mbali na wewe. Ila maandiko yasema yuko pamoja na sisi mwanzo hata mwisho fuata neno linasema nini wala si fikra zako zinasema nini na mazingira.) sio sababu ya wewe kujiachia katika uovu. Na kutembea kama unavyotaka wewe.
Maandiko yanasema asije akaturarua na asipatikane kabisa wa kuponya kwa sababu ya kuzoelea maovu na kuona Mungu ni Kama wewe jinsi unavyofikiri na kutenda la!. Tembea ba Kristo vyema katika kipindi hiki wala usijisahau kabisa.
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.