Author : Rehema Jonathan

Neno Sharoni maana yake ni “uwanda” au “nchi tambarare”. Katika maandiko tunaona kuna eneo(wilaya) ambalo linajulikana na kufahamika sana na waisraeli kama sharoni ijapokuwa katika biblia hakuna maelezo mengi yaliyotolea kuhusu eneo hilo. Ingawa ni eneo ambalo lilikuwa na rutuba nyingi, na pia lipo karibu sana na fukwe za bahari kubwa ya Mediterenia , waweza ..

Read more

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. Watu wajikatao wanaozungumziwa hapa ni Wayahudi yaani wafanyao TOHARA. Ambacho ni kitendo cha kukata sehemu ya mbele ya viungo vya uzazi vya mwanaume. Sasa hawa wajikatao yaani Wayahudi walikuwa wakiwataabisha watu na kuwashurutisha watu ambao sio Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo. Wakiwataka wafanyiwe tohara kama jinsi torati ilivyoagiza ..

Read more

Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”. Mahali hapa Mungu alitutaka tujue sifa za mtu mwenye haki, au tabia ya mtu mwenye haki mara nyingi huwa na huruma kwa Kila kitu, na huwa haishii kuonyesha huruma kwa wanadamu tu bali hata kwa wanyama pia Na ndiyo ..

Read more

Bwana Yesu asifiwe, karibu tena tujifunze Neno la Mungu kama maandiko matakatifu yanavyosema katika zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. Kuligana na swali letu ili tuweze kuelewa zaidi tusome kwanza kifungu hiki Ufunuo 21:8 “BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na ..

Read more

Ukisoma katika kitabu cha yoshua watu hawa wametajwa Yoshua 15:13 [13]Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni). Waanaki walikuwa jamii ya watu warefu na wakubwa waliotoka  katika uzao wa mtu mmoja  anayeitwa  anaki ..

Read more

Kipindi Bwana Yesu yupo hapa duniani kulikuwa na madhehebu mawili tu katika uyahudi ambayo yalikuwa Mafarisayo na Masadukayo Matendo 5:17 “Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,” Tukisoma na matendo 15 inawaelezea Mafarisayo tusome Matendo 15:5 “Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, ..

Read more

Nakusalimu kupitia Jina lipitalo majina yote JINA LA YESU , Karibu katika kujifunza neno la Mungu litupalo uzima wa milele katika maisha yetu. kuligana na swali hapo, biblia iliposema bila kazi ya mikono, Maana yake ni kuwa kitu chochote kilichotenhenezwa pasipo kitengemezi chochote, kiuhalisi katika maisha yetu, mfano kama mtu anahitaji kitu chochote kwa ajili ..

Read more

Katika maandiko bublia inafunua kuwa Bwana Yesu alianza huduma yake akiwa na umri wa miaka 30. Sasa ili tuweze kujua alikufa akiwa na umri gani, tunahitaji kujua kwanza utumishi wake ulikuwa wa miaka mingapi. Kulingana na kitabu cha Yohana, Yesu alihudhuria sikukuu tatu za Pasaka, ambazo zilikuwa za mwaka baada ya mwaka. Tukizijumlisha, tunapata jumla ..

Read more

Mikono iliyotaka ni mikono isiyokuwa na hila au dosari yeyote, yaani mikono ambayo ni safi iliyotakata 1Timotheo 2:8 “Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano” Mikono yenye hila au dosari nyenyewe inakiwaje, tusome Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; ..

Read more

Ili tuweze kuelewa mstari huu tutazame mfano huu ambao ni uhalisia wa maisha ulivyo ambao sasa utatusaidia kuelewa maana ya (Mithali 11:26) Kuna kipindi baadhi ya mikoa ya Afrika mashariki (Tanzania ) kulitokea shida ya maji, ilifanya watu kutoka umbali mrefu kwenda kutafuta maji ili waweza kufanikisha shughuli zote zinazohitaji maji, lakini sasa katika kipindi ..

Read more